array(0) { } Radio Maisha | Moses Kuria amshtumu Raila kwa madai ya kuchangia masaibu ya Miguna Miguna
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Moses Kuria amshtumu Raila kwa madai ya kuchangia masaibu ya Miguna Miguna

Moses Kuria amshtumu Raila kwa madai ya kuchangia masaibu ya Miguna Miguna

Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria amemshtumu Kinara wa ODM Raila Odinga kwa kusema amechangia masaibu yanayomkumba wakili Miguna Miguna ambaye amezuiliwa na serikali kurejea nchini.

Akizungumza na wanahabari katika Majengo ya Bunge hapa Jijini Nairobi, Kuria amesikitia hali ambapo Raila alimhusisha Miguna katika mipango yake ya kujiapisha mwezi Januari mwaka wa 2018 ilhali amenyamazia suala la kuhangaishwa kwake.

Wakati uo huo Kuria ameikosoa serikali kwa kukiuka agizo la mahakama la kutaka ifanikishe kurejea kwa Miguna huku akiwashauri Kenyatta na Raila kutumia ushirikiano wao kumrejesha wakili huyo.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya Kiongozi wa wengi katika Bunge la Seneti Kipchumba Murkomen na Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa kutoa kauli sawa na hiyo.

Ikumbukwe Miguna wakati wa mahojiano na idhaa moja ya humu nchini, alielezea kukerwa na hatua hiyo akidai Meneja wa Kampuni ya Ndege ya Lufthansa alimzuia kuabiri ndege hiyo kutokana na masharti aliyopewa na serikali ya Kenya.