×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Magavana watofautiana na DPP kuhusu hatua ya Sonko kumteua naibu wake

Magavana watofautiana na DPP kuhusu hatua ya Sonko kumteua naibu wake

Mvutano umeibuka baina ya Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu Mashtaka ya Umma DPP na Uongozi wa Serikali za Kaunti  baada ya Baraza la Magavana kutofautiana na kauli ya Noordin Haji kuhusu uteuzi wa Naibu Gavana wa Kaunti ya Nairobi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mapema leo, Baraza la Magavana limesema kuwa Sonko alitekeleza jukumu lake kwa mujibu wa sheria za uongozi wa kaunti kumteua naibu wake na kwamba hakukiuka sheria yoyote, kinyume na DPP alivyosema kuwa Sonko alikiuka sheria hasa baada ya mahakama kumzuia kufika ofisini kufuatia kesi ya ufisadi inayomkabili.

Aidha akimjibu Haji mapema leo, katika barua yake kwa Noordin Haji, Sonko amesisitiza kwamba hakukiuka masharti yoyote ya dhamana aliyopewa na mahakama kwa mumtea Ann Kananu Mwenda kuwa naibu wake, akidai kuwa mashrati hayo yalimzuia kuingia ofisini na wala si kutekeleza majukumu yake.

Sonko ambaye alijibiwa muda mchache na Haji baada ya kumteua Ann Mwenda kuzuia kuingia ofisini hakumaanisha kwamba Kaunti ya Nairobi haina gavana, akitoa mfano wa uamuzi wa Mahakama ya Kiambu katika kesi ya Gavana wa Fardinard Waititu ambapo iliamuru kwamba licha ya Waititu kuzuiwa kufika ofisini, bado anajukumu la kutekeleza majukumu yake jinsi yalivyooredheshwa kwenye katiba.

Jumatatu wiki hii katika taarifa iliyowashangaza wengi, Sonko alimteua Ann Mwenda kuwa naibu wake na hivyo kuchangia kuwapo kwa mijadala mitandaoni kuhusu hatua hiyo.

Aidha kinaya kikubwa kilichofuatia kwamba siku kadhaa baada ya uteuzi huo, Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi na aliyekuwa Kiongozi wa Wengi katika bunge hilo Abdi Guyo waliamua kuweka kando tofauti zao na kuahidi kushirikiana kuukabili ufisadi katika serikali ya Nairobi.

Hata hivyo suala ambalo liliibua mjadala kuhusu iwapo Elachi bado yu katika upande wa Sonko ni pale ambapo alisema wameamua kushirikiana kuhakikisha kuwa mawaziri na wafanyakazi wengine waliosimamishwa kazi na Sonko wanarejea kazini. kinachosubiriwa sasa ni iwapo DPP atawasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya Sonko.