array(0) { } Radio Maisha | Wanafunzi elfu tisa waliofanya vyema katika KCPE kunufaika kupitia ufadhili wa serikali
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanafunzi elfu tisa waliofanya vyema katika KCPE kunufaika kupitia ufadhili wa serikali

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha ameongoza uzinduzi rasmi wa mpango wa ufadhili wa wanafunzi kwa jina Elimu Scholarship Programme ambao unalenga kuwafadhili watahiniwa elfu tisa waliofanya vyema katika Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane, KCPE mwaka uliopita. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Magoha ameusifu mpango huo wa ufadhili akisema utawanufaisha pakubwa watoto kutoka familia maskini.
 
Aidha ametoa changamoto kwa wabunge ambao hutoa ahadi za kuwafadhili wanafunzi kupitia hazina ya CDF akisema wanastahili kutumia busara katika uteuzi  ili kuhakikisha wanafunzi wanaohitaji usaidizi ndio wanaonufaika.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Belio Kipsang amesema mikakati zaidi inaendelea ili kuhakikisha wanafunzi wanaohitaji ufadhili wa masomo wananufaika.
 
Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Equity, James Mwangi aidha ameelezea ufanisi ambao umeshuhudiwa awali kupitia ufadhili wa wanafunzi katika mpango wa Wings to Fly , akisema ufanisi zaidi unatarajiwa kupitia Elimu Scholarship , ambao ni mpango wa ufadhili unaoendelezwa na serikali kutokana na ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu na Wakfu wa Benki ya Equity.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa, Julius Melly ambaye pia ni Mbunge wa Tinderet, kwa upande wake ameipongeza serikali kwa juhudi zake za kusambaza vitabu vya kiada katika shule mbalimbali nchini huku akiipa changamoto kuelekeza juhudi zake sasa katika usambazaji wa vifaa vya maabara katika shule za umma. Aidha ameitaka serikali kusambaza fedha shuleni kwa wakati ufaao ili kutotatiza shughuli za masomo.
 
ambao unalenga kuwafadhili watahiniwa elfu tisa waliofanya vyema katika Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane, KCPE mwaka uliopita. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Magoha ameusifu mpango huo wa ufadhili akisema utawanufaisha pakubwa watoto kutoka familia maskini.