array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wanne wa ujambazi wauiliwa Eldoret

Washukiwa wanne wa ujambazi wauiliwa Eldoret

Washukiwa wanne wa ujambazi wauiliwa Eldoret

Maafisa wa polisi mjini Eldoret wamewaua kwa kuwapiga risasi washukiwa wanne wanaoaminika kuwa majambazi sugu.

Wanne hao wameuliwa kwenye Barabara Kuu ya Uganda walipokuwa wakiingia mjini Eldoret kwa gari dogo. Inaarifiwa kwamba washukiwa wamekuwa wakijihusisha na wizi wa kimabavu na wamekuwa wakisakwa kwa muda.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Uasin Gishu Johnston Ipara wanne hao walinuia kulivamia eneo moja la kibiashara asubuhi ya leo kabla ya kufumaniwa na polisi na kuualiwa.

Polisi wamepata bastola moja na risasi 11 pamoja na vifaa viwili vya kuwekea risasi  kwenye gari ambalo wanne hao walikuwa wakisafiria.

Ipara ameahidi kukabili  visa vya uhalifu ambavyo vimekithiri mjini Eldoret ,akiwaonya wahalifu ambao wanalenga kuendeleza shughuli zao mjini humo.

Aidha amewataka wale wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kwa idara ya polisi.