array(0) { } Radio Maisha | Ndege yaanguka ikiwa na abiria 180 nchini Iran

Ndege yaanguka ikiwa na abiria 180 nchini Iran

Ndege yaanguka ikiwa na abiria 180 nchini Iran

Shirika la Habari la Iran limesema kwamba hakuna dalili yoyote ya manusura wa mkasa wa ndege aina ya Boeing 737 iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Imam Khomeini katika jiji kuu la Iran, Tehran.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria180 pamoja na wahudumu wengine na ailianguka dakika chache tu baada ya kupaa huku idara ya usalama nchini humo imesema kwamba ndege hiyo imeanguka kutokana na hitilafu ya kimitambo.