array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wawili waliotekeleza shambulizi eneo na Saretho Garissa wameuliwa

Washukiwa wawili waliotekeleza shambulizi eneo na Saretho Garissa wameuliwa

Washukiwa wawili waliotekeleza shambulizi eneo na Saretho Garissa wameuliwa

Maafisa wa usalama wamefanikiwa kuwaua washukiwa wawili wa Kundi la Kigaidi la Al Shabaab waliohusika katika shambulizi eneo la Saretho, Garissa mapema leo. Kwa mujibu wa taarifa ya Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai, kupitia kwa afisa wa mawasiliano, Charles O Wahong'o, bunduki mbili aina ya AK 47 zimepatikana kutoka kwa wavamizi hao, vifaa vya kutengeneza vilipuzi na silaha nyingine.

Watu wanne waliuliwa wakati wa shambulio hilo miongoni mwao mwalimu na mtoto mchanga. Shambulio hilo lilitekekezwa mwendo wa saa nane  unusu  usiku wa kuamkia leo huku mnara wa mawasiliano wa Kampuni ya Safaricom ukiharibiwa.

Polisi wamefaulu kudhibiti hali huku usalama ukiimarishwa. Shambulio hili limejiri siku chache tu baada ya jingine katika eneo la Manda Bay, Kaunti ya Lamu ambako mwanajeshi mmoja wa Marekani na wafanyakazi wengine wawili raia wa taifa hilo waliuliwa.