array(0) { } Radio Maisha | Miguna Miguna azuiliwa tena kuja Kenya

Miguna Miguna azuiliwa tena kuja Kenya

Miguna Miguna azuiliwa tena kuja Kenya

Wakili Miguna Miguna amezuiliwa kuabiri ndege aliyonuia kusafiria kutoka Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, Ujerumani kuja Kenya.

Akihojiwa na idhaa moja humu nchini, Miguna ameeleza kusikitishwa kwake na hatua hiyo akisema kwa meneja wa Kampuni ya Ndege ya Lufthansa alimzuia kuabiri ndege hiyo akisema walipewa masharti ya kutomsafirisha kuja nchini Kenya au taifa lolote la Bara Afrika.

Aidha, Miguna amesema kwamba Ndege ya Lufthansa imetoa sharti kwamba Serikali ya Kenya lazima itume ujumbe kwa ofisi yao Jijini Frankfurt kabla ya wao kuweza kumsafirisha Miguna kuja Kenya au taifa lolote Barani Afrika.