array(0) { } Radio Maisha | Marekani yathibitisha kwamba wafanyakazi wake watatu waliuliwa wakati wa shambulio la kigaidi eneo la Manda Bay.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Marekani yathibitisha kwamba wafanyakazi wake watatu waliuliwa wakati wa shambulio la kigaidi eneo la Manda Bay.

Marekani yathibitisha kwamba wafanyakazi wake watatu waliuliwa wakati wa shambulio la kigaidi eneo la Manda Bay.

Marekani imethibitisha kwamba wafanyakazi wake watatu waliuliwa wakati wa shambulio la kigaidi katika eneo la Manda Bay, Kaunti ya Lamu.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wake, taifa hilo limesema kwamba waliouliwa ni mmoja wa wanajeshi wake na wengine wakiwa wafanyakazi waliokuwa kwenye kandarasi. Aidha, imedokeza kwamba maafisa wengine wawili walijeruhiwa na tayari wamesafirishwa kutoka Lamu ili kutibiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotiwa saini na Kamanda wa Kikosi cha US AFRICA, Generali Stephne Townsend, waliojeruhiwa wanaendelea kupata nafuu na kusisistiza kwamba kamwe halikuwatikisha na kwamba mikakati ipo ya kulikabili kikamilifu kundi hilo la kigaidi. 

Wanachama watano wa Al Shabaab waliuliwa wakati wa makabiliano hayo huku zana za kivita ikiwamo bendera ya kundi hilo haramu ikipatikana .

Wakati wa shambulio hilo la alfajiri, wanachama wa kundi hilo waliingia kwenye kambi hiyo ya kijeshi kwa jina Simba Camp kabla ya kuwavamia wanajeshi wa Kenya kwa ushirikiano na wenzao wa Marekani. Ndege moja ya Marekani iliteketezwa wakati wa tukio hilo.