array(0) { } Radio Maisha | Magaidi wa Shabaab wauliwa wakivamia Uwanja wa Ndege Lamu huku 4 wakuliwa na KDF
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Magaidi wa Shabaab wauliwa wakivamia Uwanja wa Ndege Lamu huku 4 wakuliwa na KDF

Magaidi wa Shabaab wauliwa wakivamia Uwanja wa Ndege Lamu huku 4 wakuliwa na KDF

 

Idara ya Jeshi la Ulinzi KDF imesema kumekuwapo na jaribio la shambulio la Kigaidi katika Uwanja wa ndege wa Manda wala si katika kambi ya Majeshi ya Marekani jinsi ilivyodaiwa na Kundi Gaidi la Al Shaabab.

Msemaji wa Idara ya Jeshi KDF Paul Njuguma amesema magadi  4 wa Al Shabaab wameuliwa asubuhi ya kuamkia leo na wanajeshi. wakati walipokuwa wakijaribu kuuvamia uwanja huo.

Kuhusu moshi ulionekana ukifuka hewani na kudaiwa kuwa ndege nne zilizoteketezwa na magaidi hao, Kanali Njuguna amekanusha habari hizo na kusema moto ulizuka katika uwanja huo baada ya matanki ya mafuta kupasuka kutokana na ufyatuliaji wa risasi baina ya wanajeshi na magaidi.

Kanali Njuguna vilevile amethibitisha kuwa usalama umeimarishwa katika maeneo yote ya Pwani kufuatia jaribio hilo la shambulio, akisema vikosi vyote vya majeshi vipo tayari na imara kuwakabili magaidi.

Taarifa ya KDF imejiri kufuatia taarifa ya Al Shabba kudai kuwa imeishambulia Kami ya Wanajeshi ya Simba kaunti ya Lamu ambayo huwa makazi ya mamia ya wanajeshi wa kenya na Marekani ambao hutoka ulinzi kwenye mpaka wa Kenya na Somali.