array(0) { } Radio Maisha | Vijana wa K-Sharks kumenyana na wanaume
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vijana wa K-Sharks kumenyana na wanaume

Vijana wa K-Sharks kumenyana na wanaume

Na Shadrack Andenga Odinga

NAIROBI, KENYA, Nahodha wa timu ya Sofapaka George Maelo ametia chumvi kwenye kidonda cha Kariobangi Sharks kabla ya mechi dhidi yao siku ya Jumamosi uwanjani Kenyatta, mjini Machakos.

Akizungumza na meza ya michezo Redio Maisha mapema Jumamosi, Maelo alikuwa mwenye motisha.

“Ni kweli tulianza msimu vibaya. Mkufunzi aliyeondoka Alves alikuwa na mfumo tofauti sana na ule ambao tumeuzoea hapa Sofapaka. Sasa baada ya yeye kuondoka na tumerejeshewa Baraza, tumecheza mechi tano bila kupoteza. Kariobangi Sharks ni timu nzuri lakini wanakosa ukomavu, bado wale ni vijana wadogo, watarajie kivumbi” alisema nahodha huyo ambaye ni beki pembeni kulia wa kupanda na kushuka huku akiongezea kwamba wanachezea sasa alama tatu pekee.

Sofapaka walianza msimu vibaya walipokuwa na mkufunzi Divaldo Alves kutoka Ureno. Msururu wa matokeo mabovu yalimkosesha rais wa timu hiyo Elly Kalekwa usingizi na akaamua kumfuta kazi. Kwa sasa ‘Batoto ba Mungu’ wako katika nafasi ya nane baada ya michuano 13 na alama 21, alama nane nyuma ya kiongozi Gormahia fc.

“ Bado tuna ndoto ya kushinda ligi msimu huu. Chochote cha weza tendeka, kwetu sisi ni kazi tu kisha tuwe na imani. Ona kwa mfano maajuzi kule Kisumu dhidi ya Western Stima, walipewa penalti dakika za mwisho ambayo haikuwa inaeleweka na mechi hiyo kuishia sare ya bao moja kwa moja. Kwa sasa katika dirisha hili fupi la uhamisho angalau tumepata wachezaji tofauti tofauti wa hapa nchini na wa kigeni ambao wanaweza kuwa na mchango mzuri ambao utatimiza ndoto yetu ya kushinda ligi. Mpira ambao tunacheza sasa niwa kiume, sisi hatutaki masihara. Wanaume wataonana kiwanjani na vijana kukaa kando.” Aliendelea Maelo huku akiwapa matumaini mashabiki wa Sofapaka fc.

Kariobangi Sharks wapinzani wa Sofapaka fc walitoka saree ya mabao matatu kwa matatu na Posta rangers fc mechi yao ya mwisho. Vijana hao wa Nick Mwendwa na mkufunzi William Muluya wameanza msimu vibaya haswa baada ya matatizo ya kiuchumi na wako katika eneo la hatari, kushushwa ligi.

Kariobangi Sharks wako katika nafasi ya 15, baada ya kucheza mechi 14 wamejizolea alama tisa pekee. Wako juu ya Kisumu all-stars ambao wana alama nane na Chemilil sugar fc ambao wanaburura mkia kwa alama moja.

Mechi yao dhidi ya Sofapaka fc niya kufa kupona maanake wanahitaji alama zote tatu ili kujitoa katika eneo la hatari kushushwa ligi. Sofapaka nao wanahitaji hizo alama tatu pia ili kujiboresha katika jedwali na kutimiza ndoto ya nahodha Maelo ya kushinda ligi.

Wawili hawa wanapo garagazana, sisi kwetu Redio Maisha nikuwatakia mema tu, aidha wawe ni vijana au wanaume, kila la heri mibabe wa KPL.