×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raia wa Marekani wahimizwa kuondoka Iraq mara moja kufuatia mauaji ya Qasem Soleiman

Raia wa Marekani wahimizwa kuondoka Iraq mara moja kufuatia mauaji ya Qasem Soleiman

Raia wa Marekani walioko taifa la Iraq, wameshauriwa kuondoka mara moja katika taifa la Iraq baada ya Marekani kumuua Meja Generali wa vuguvugu la Islamic Revolutionary Guard Corps la Iran Qasem Soleimani mapema leo katika uwanja wa ndege wa Baghdad.

Vilevile Marekani imewaonya raia wake walioko Iraq kutofika katika ubalozi wa  Marekani nchini humo baada ya ubalozi huo kuvamiwa siku ya Jumanne wiki hii kufuatia kuuliwa kwa wanajeshi wa kundi la Hezbollah. Shambulio hilo la Hezbollah lilitokea baada ya raia wa Marekani kuuliwa katika taifa la Iraq.

Haya yanajiri huku Baraza Kuu la Usalama Nchini Iran likisubiriwa kutoa taarifa rasmi ndani ya saa moja ijayo kuhusu hatua itakayochukuliwa dhidi ya Marekani.

Inaarifiwa kuwa Qasem na wenzake walikuwa wakiondoka katika uwanja huo wakitumia magari mawili waliposhambuliwa na ndege za kijeshi za Marekani zisizokuwa na rubani.

Kwa mujibu wa Marekani,  mauaji hayo yanalenga kuzuia mashambulizi kutoka kundi hilo la Iran. Hata hivyo,  Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Iran Javad Zarif katika mtandao wake wa twitter , amekashifu vikali mauaji hayo akisema Marekani itawajibikia matokeo.

Mauaji hayo yamepandisha bei ya mafuta kwa asilimia nne.