array(0) { } Radio Maisha | Huenda mauaji ya Qasem yakaleta mvutano baina ya Marekani na Iran

Huenda mauaji ya Qasem yakaleta mvutano baina ya Marekani na Iran

Huenda mauaji ya Qasem yakaleta mvutano baina ya Marekani na Iran

Mvutano mkali unatarajiwa baina ya Marekani na Iran, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuagiza mauaji ya Meja Generali wa vuguvugu la Islamic Revolutionary Guard Corps la Iran Qasem Soleimani mapema leo katika uwanja wa ndege wa Baghdad.

Inaarifiwa kuwa Qasem na wenzake walikuwa wakiondoka katika uwanja huo wakitumia magari mawili waliposhambuliwa na ndege za kijeshi za Marekani zisizokuwa na rubani.

Kwa mujibu wa Marekani,  mauaji hayo yanalenga kuzuia mashambulizi kutoka kundi hilo la Iran. Hata hivyo,  Waziri wa Masuala ya Nje wa Iran Javad Zarif katika mtandao wake wa twitter ,amekashifu vikali mauaji hayo akisema Marekani itawajibikia matokeo.

Mauaji hayo yamepandisha bei ya mafuta kwa asilimia nne.