array(0) { } Radio Maisha | Wizara ya Afya: Mikakati ya kutatua Masaula ya kiakaili yaanza

Wizara ya Afya: Mikakati ya kutatua Masaula ya kiakaili yaanza

Wizara ya Afya: Mikakati ya kutatua Masaula ya kiakaili yaanza

Miezi sita tu baada Rais Uhuru Kenyatta kuagiza Wizara ya Afya kushugulikia suala la afya ya kiakili kwa kuweka mikakati ya kupunguza visa vya watu kujiua, Wizara hiyo imetoa ratiba ya jinsi itakavyoshughulikia huduma za afya akili kuanzia mwezi huu, baada ya kubuni jopo kazi  mapema mwezi uliopita.  

Jopo kazi hilo litakaloongozwa na mtaalam wa Masula ya Akili dakta Frank Njenga litafanya kikao na umma katika eneo la Embu tarehe 13 mwezi huu kabla ya kuelekea Kaunti ya Makueni tarehe 14, tarehe 15 Eldoret, tarehe 16 Nakuru, Kakamega tarehe 17, Kisumu tarehe 20, Nyeri 21, Garissa 22, Mombasa tarehe 23 kisha Nairobi tarehe 27amabpo ripoti kamili itakusanywana kuwasilishwa kwa Wizara ya Afya.

Yanayotarajiwa kujadiliwa ni matumizi mabaya ya dawa za kulevya, michezo ya bahati nasibu, visa vya ubakaji na dhuluma za kijinsia pamoja unyanyasaji wa watoto.

Katika hotuba yake mwaka jana, Rais Kenyatta alitoa wito kwa yeyote aliye na mafadhaiko kutafuta ushauri nasaha au kuzungumza na yeyeote wa karibu unayemwamini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani, WHO mwaka wa 2014 Kenya iliorodheshwa ya 4 Barani Afrika kwa kuwa na watu milioni 1.9 wenye matatizo ya kiakili kufuatia msongo wa mawazo.

Vilevile mwaka 2016 ripoti ya WHO ilionesha kuwa nchini Kenya visa 142, 520 vya wanaojaribu kujiua viliripotiwa, ambapo visa vya kujaribu kujiua ni mara 20 zaidi ya vya visa vya watu kujiua.