array(0) { } Radio Maisha | Nzige wa Jangwani wavamia tani milioni1.8 za kilimo kila siku

Nzige wa Jangwani wavamia tani milioni1.8 za kilimo kila siku

Nzige wa Jangwani wavamia tani milioni1.8 za kilimo kila siku

Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi baada ya Nzige wa Jangwani yaani Desert Locust kuivamia mimea kwenye sehemu hiyo kuanzia siku ya Jumapili. Wakazi wameelezea wasiwasi wao huku viongozi na wataalamu wakiahidi kuweka mikakati ya kukabili hali hiyo. Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Nzige hao kuyavamia maeneo hayo huku Umoja wa Mataifa UN ukieleza madhara yanayoweza kuletwa na Nzige hao vilevile mataifa ambayo yameathirika pakubwa kufikia sasa.

Tangu siku ya Jumapili wakazi wa maeneo ya Kaskazini mwa Nchi wamelalamikia uvamizi wa Nzige ambao ambao athari yake inaendelea kuongezeka kwa kuathiri mimea.

Hata hivyo uvamizi huo haujafanyika ghafla kwani mwezi uliopita Shirika la Umojawa Mataifa la Kilimo na Chakula FAO lilionya kuwa Nzige hao wangesambaa katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki baada ya kuvamia mataifa ya Ethiopia na Somalia.

Kwa mujibu wa FAO Nzige hao walivamia tani milioni 1.8 za kilimo kila siku katika taifa la Ethiopia. Wadudu hao waliingia nchini humu kutoka Somalia na kuanza kuvamia eneo la Kotulo katika Kaunti ya Wajir.

Mbunge wa Eldas Aden Keynan, amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa UN, imeonesha kuwa mataifa ya Sudan, Ethiopia, Yemen, India, Pakistan na mataifa ya Afrika Mashariki yameathirika pakubwa na uvamizi huo.

Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Kaunti ya Wajir, siku ya kwanza Nzige hao walivamia zaidi ya kilomita 30 ya kilimo, akisema baadhi ya wakazi walijaribu wawezavyo kuwafukuza kwa kupiga kelele, kugonga vyuma na honi za magari ili kuwashtua bila kufua dafu, huku wengine wakiamua kusoma Quran na kuomba.

Mtaalamu wa masuala ya mazingira, anaelezea kwamba mabadiliko ya hali ya anga yamechangia pakubwa uvamizi wa nzige hao.

FAO imesema Nzige hao hupeperuka kilomita 150 kila siku, ambapo kundi la Nzige milioni 40 kwa siku wanaweza kuharibu mazao yanayoyoweza kuwalisha watu elfu 35, Ngamia 20 na Ndovu sita.Kundi moja pekee la Nzige hao wameharibu chakula kinachoweza kuwalisha takriban watu 2,500 kwa mwaka.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza Nzige hao wa Jangawani kuvamia maeneo ya Kaskazini mwa Nchi mwaka wa 2007 vilevile kisa hicho kiliripotiwa kabala ya kudhibitiwa, nakama ilivyo sasa Nzige hao waliingia Nchini kutoka mataifa ya Somalia na Ethiopia.