array(0) { } Radio Maisha | Marekani yawaua magaidi wa Al Shabaab

Marekani yawaua magaidi wa Al Shabaab

Marekani yawaua magaidi wa Al Shabaab

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Serikali ya Marekani imesema kwamba imefanikiwa kuwaua magaidi wanne wa kundi la Al Shabaab katika mashambulio ya angani yaliyotekelezwa jana nchini Somalia.

Aidha, imesema kwamba mashambulio hayo yametekelezwa katika maeneo mawili ambayo yanaaminika kuwa ngome ya kundi hilo ambalo mwishoni mwa wiki iliyopita lilitekeleza shambulio lililotajwa kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Aidha, Marekani imeahidi kuendeleza vita dhidi ya Al Shabaab pamoja na kuhakikisha halitekelezi shambulio lingine.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya watu sabini waliuliwa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa wakati wa shambulizi hilo wengi wakiwa wanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Somalia.