array(0) { } Radio Maisha | Ada ya ksh400 kuendelea kutozwa Jijini Nairobi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ada ya ksh400 kuendelea kutozwa Jijini Nairobi

Ada ya ksh400 kuendelea kutozwa Jijini Nairobi

Na Victor Mulama,

NAIROBI, KENYA, Serikali ya Kaunti ya Nairobi itaendelea kutekeleza ada mpya ya shilingi mia nne za kuegesha magari jijini Nairobi, hadi kesi inayopinga ada hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Hatua hiyo inajiri baada ya Jaji James Makau kusema upande wa mlalashi katika kesi hiyo ambapo ni Chama cha Kutetea Maslahi ya Wateja, COFEK, kukosa kuwasilisha matakwa yake ya kutaka ada hiyo isitishwe jinsi inavyohitajika kisheria.

Jaji Makau amesema ni vigumu kufahamu iwapo COFEK ilitaka ada hiyo kusitishwa kwa magari ya binafsi au ya uchukuzi wa umma.

Makau ameishauri COFEK kuhakikisha inapanga kisheria matakwa yake kabla ya kuyawasilisha mahakamani pamoja na kutuma nakala za matakwa hayo kwa kaunti ya Nairobi ili kurahisisha kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kesi hiyo itaendelea kusikizwa tarehe 17 mwezi Februari mwaka 2020.

Ikumbukwe Tarehe 12 mwezi huu Mahakama Kuu ya Nairobi ilitoa agizo la kusitisha tangazo la kuongeza ada hiyo baada ya COFEK kuwasilisha kesi ya kuipinga.

COFEK iliwasilisha kesi hiyo baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Uegeshaji katika Kaunti ya Nairobi Tom Tinega, kutangaza ada mpya ya shilingi mia nne kuwa ya kuegesha magari ili kupunguza msongamano jijini.