×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Afisa wa GSU akamatwa kwa utekaji nyara, Malindi

Afisa wa GSU akamatwa kwa utekaji nyara, Malindi

Washukiwa watatu wa utekaji nyara wanaendelea kuzuilia jijini Mombasa baada ya kukamatwa mapema leo na Maafsia wa Idara ya Upelelezi DCI . Washukiwa hao wanatuhumiwa kumteka nyara mfanyakazi wa kampuni ya Safaricom tawi la Malindi.

Inaarifiwa mfanyakazi huyo alikuwa amechukua mkopo wa shilingi nusu milioni kutoka kwa mmoja wa washukiwa kwa jina Grace Wairimu na akakosa kulipia jinsi walivyokubaliana.

Polisi wanasema washukiwa walimvamia mwanamke huyo katika eneo lake la kazi na kumlazimu kuingia ndani ya gari la binafsi kisha kutoweka naye.

Hata hivyo polisi walifanikiwa kumwokoa mwathiriwa huku wakianzisha uchunguzi.