array(0) { } Radio Maisha | Watu zaidi ya 90 wafariki kufuatia mlipuko wa bomu, Somalia
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu zaidi ya 90 wafariki kufuatia mlipuko wa bomu, Somalia

Watu zaidi ya 90 wafariki kufuatia mlipuko wa bomu, Somalia

Idadi ya watu ambao wamefariki dunia kufuatia mlipuko wa bomu la kutegwa garini nchini Somalia imefika watu tisini. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa serikali nchini humo ni kwamba, watu wengine zaidi ya sitini wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea viungani mwa Jiji la Mogadishu. 

Mmoja wa wabunge nchini humo kwa jina Abdirazak Mohammed amesema miongoni mwa waliouliwa ni maafisa kumi na saba wa polisi,  na raia wanne wa taifa la  Uturuki. Aidha basi lililokuwa na wanafunzi zaidi ya ishirini wa Chuo Kikuu cha Benadir limeharibiwa huku wanafunzi kadhaa wakifariki dunia.

Mlipuko huo umetokea barabarani katika eneo la kuyakagua magari huku nyumba zilizo karibu vilevile zikiharibiwa. Hakuna kundi limekiri kuhusika katika shambulio hilo kufikia sasa.