array(0) { } Radio Maisha | KWISHA, LIGI ISHATUTOKA, PEP ASALIMU AMRI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KWISHA, LIGI ISHATUTOKA, PEP ASALIMU AMRI

KWISHA, LIGI ISHATUTOKA, PEP ASALIMU AMRI

Mkufunzi wa Manchester City Josep Guardiola amekiri ya kwamba ligii kuu ingereza EPL kwa sasa iko mikononi mwa Liverpool fc.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Wolverthampton Uingereza baada ya kichapo cha mabao matatu kwa mawili na wenyeji Wolves fc usiku wa ijumaa, Guardiola alihuzunikia hali yake.

“Liverpool kwa sasa wana nafasi kubwa sana. Hilo pengo la alama kati yetu na wao ni kubwa sana. Kwa sasa sisi tunafikiria kuhusu Leicester City fc, sio Liverpool. Nikisema kuhusu Liverpool basi nitakuwa mwongo, si hali ambayo ina uhai wowote ile, ila ni ndoto tu kwa sasa. Kutetea ubingwa wetu wa EPL itakuwa vigumu kwa sasa, japo nafasi bado ipo, ni finyu.” Alisema Guardiola huku akionekana kuwa katika hali ya kuchanganikiwa baada ya kuwa uongozini kwa idadi ya mabao mawili ambayo yalikombolewa katika kipindi cha pili, kisha baadaye wenyejeji wakapata la ushindi.

Raheem Sterling ambaye alipachika wavuni mabao mawili ya kwanza katika mechi hiyo, kwa sasa ameiweka rekodi mpya katika taaluma yake. Ni mara ya kwanza yeye kupoteza mechi ambayo amefunga bao ama mabao akiichezea Man City katika EPL.

“ Kwa sasa tuko katika hali ngumu. Sijui kilicho tokea, lakini hatukutarajia haya. Ligi bado iko mikononi mwetu japo Liverpool wana mafao makubwa. Lakini bado tuna imani, hatutakata tamaa.” Alisema Sterling baada ya mechi hiyo huku akijaribu kujipatia matumaini.

Man City kwa sasa wako katika nafasi ya tatu katika jedwali la EPL, alama 14 nyuma ya viongozi Liverpool fc. Vijana hao wa Pep kwa sasa pia wamepoteza ujumla wa mechi tano katika ligi. Ikumbukwe ya kwamba pia Man City wamecheza mechi moja zaidi ya Liverpool ambao wamepoteza alama mbili peke yake msimu huu.

Liverpool pia, kwa mechi 27 za EPL kwanzia mwezi Machi, wamepata ushindi wa mechi 26 na iwapo watashinda mechi mbili zifuatazo katika EPL, basi watakuwa na rekodi ya kucheza mwaka wa 2019 wote bila kushindwa mechi yeyote ya EPL.