array(0) { } Radio Maisha | Mwanamke afariki dunia baada ya kukanyagwa na ndovu mpakani pa Laikipia na Baringo

Mwanamke afariki dunia baada ya kukanyagwa na ndovu mpakani pa Laikipia na Baringo

Mwanamke afariki dunia baada ya kukanyagwa na ndovu mpakani pa Laikipia na Baringo

Shirika la Huduma za Wanyapori, KWS limeeleza kusikitishwa na kisa ambapo mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya kukanyagwa na ndovu katika Msitu wa Ol Arabel mpakani pa kaunti za Laikipia na Baringo.

Katika taarifa, KWS imesema kwamba mwanamke huyo mwenye umri wa miaka thelathini na sita kwa jina Stella Chebii, alikuwa amekwenda katika msitu huo kuwatafuta mifugo wake waliopotea wakati alipovamiwa na ndovu. Mwili umepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Nyahururu.

KWS aidha imesema imebuni kikundi maalum cha maafisa wake kufuatilia mienendo ya ndovu ambao wamejaa katika eneo hilo ili kudhibiti mizozo baina yao na binadamu. Wakazi wa eneo hilo aidha wameombwa kuwa makini hasa wanapoyakabiria maeneo yenye misitu ili kuepusha visa vya kuvamiwa na wanyamapori.