array(0) { } Radio Maisha | Abiria kumi wafariki dunia katika ajali ya ndege nchini Kazakhstan

Abiria kumi wafariki dunia katika ajali ya ndege nchini Kazakhstan

Abiria kumi wafariki dunia katika ajali ya ndege nchini Kazakhstan

Abiria zaidi ya kumi wamefariki dunia leo asubuhi baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Almaty nchini Kazakhstan, eneo lililo katikati ya Asia. Kwa mujibu wa serikali ya taifa hilo, ndege hiyo ilikuwa na abiria mia moja pamoja na wafanayakazi watano.

Abiria kadhaa walijeruhiwa wakati wa kisa hicho. Rais wa taifa hilo, Kassym-Jomart Tokayev ameahidi kuzifidia familia ambazo jamaa zao wameathirika katika mkasa huo. Aidha, uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.