array(0) { } Radio Maisha | Ole Kina aunga mkono matumzi ya kamera za kunasa matukio barabarani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ole Kina aunga mkono matumzi ya kamera za kunasa matukio barabarani

Ole Kina aunga mkono matumzi ya kamera za kunasa matukio barabarani

Baada ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji kupendekeza kwamba polisi wa trafiki wanastahili kupewa kamera maalum ili kuwawezesha kurekodi visa vya uhalifu, sasa maseneta wameunga mkono pendekezo hilo.

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina amesema atapendekeza mabadiliko katika sheria za trafiki ili kuhakikisha kwamba magari yote ya uchukuzi wa umma yanakuwa na kamera na madereva kusalia garini katika vizuizi vyote vya barabarani na wakati polisi wanapofanya ukaguzi. Aidha katika mapendekezo hayo Seneta Ole Kina anataka maafisa wa polisi kuzuiwa kuingia ndani ya magari ya binafsi.

Mapendekezo haya yanalenga kupunguza ufisadi miongoni mwa maafisa hao wa trafiki.

Jumatano wiki hii Haji alipendekeza kuwa magari hayoyanastahili kuwa na kamera ili kuwasaidia polisi kukusanya ushahidi. Pendekezo hili lilijiri baada ya Ispekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kuonya kwamba abiria watakaopatikana wamepanda gari ambalo tayari limejaa watashtakiwa. Hata hivyo Haji, alifafanua kwamba itakuwa vigumu kuwashtaki abiria kwa kuwa itakuw avigumu kupata ushahidi.