array(0) { } Radio Maisha | Mutua asema yu tayari kuiongoza jamii ya Wakamba kuwania urais 2022
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mutua asema yu tayari kuiongoza jamii ya Wakamba kuwania urais 2022

Mutua asema yu tayari kuiongoza jamii ya Wakamba kuwania urais 2022

Gavana wa Machakos Alfred Mutua sasa anawataka Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama kukoma kuipotosha jamii ya Wakamba. Akiwahutubia wanahabari baada ya checeh za maneno kuibuka baiana ya Kalonzo na Muthama, Mutua amesema kwamba inasikitisha kuona kwamba viongozi hao ambao wamekuwa siasani kwa muda mrefu hawana misimamo.

Mutua amewakosoa viongozi hao wawili akisema hawana haja na manufaa ya wakazi akisema wanajitafutia nyadhfa.Awali baadhi ya viongozi wa Chama cha Wiper walimkosoa vikali Muthama kwa kutomheshimu kiongozi wa Chama hicho Kalonzo Musyoka, huku wakimtaka ajiondoe chamani iwapo hakubaliani naye.

Malumbano hayo yalianza mapema wiki hii wakati ambapo Kalonzo alisema ataendelea kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta huku Muthama akisema msimamo huo hauna mwelekeo ikizingatiwa Rais Kenyatta anahudumu katika muhula wake wa mwisho na atasaafu mwaka 2022.