array(0) { } Radio Maisha | Mwanamke afariki baada ya kupigwa na nguvu za umeme Kibra

Mwanamke afariki baada ya kupigwa na nguvu za umeme Kibra

Mwanamke afariki baada ya kupigwa na nguvu za umeme Kibra

Mwanamke mmoja amefariki dunia katika eneo la Laini Saba Mtaani Kibera baada ya kupigwa na nguvu za umeme. Inaarifiwa kwamba mwanamke huyo alipigwa na umeme wakati alipokwenda kuoga katika bafu moja ya umma eneo la Amref mtaani humo.

Mkuu wa Polisi Utawala katika eneo la Kibra, Andrew Musaisi amesema tayari maafisa wa Kampuni ya Kenya Power wamefahamishwa kuhusu tukio hilo na kutakiwa kukatiza umeme ili kutoa nafasi ya kuondolewa kwa mwili wa mwanamke huyo.