array(0) { } Radio Maisha | Watu 2 wafariki dunia katika ajali eneo la Southern By Pass

Watu 2 wafariki dunia katika ajali eneo la Southern By Pass

Watu 2 wafariki dunia katika ajali eneo la Southern By Pass

Watu wawili wameaga dunia katika barabara ya Southern Bypass jijini Nairobi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori lililokuwa limeegeshwa barabarani. Ajali hiyo imetokea karibu na makutano ya barabara ya Ngong na hiyo ya Southern Bypass.

Ajali nyingine imeripotiwa kutokea katika barabara ya Mombasa karibu na eneo la Syokimau. Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya gari la abiria kubingiria baada ya kugongana na jingine.