array(0) { } Radio Maisha | Mgando wa damu ulisababisha kifo cha Jaji James Odek. upasuaji wabainisha

Mgando wa damu ulisababisha kifo cha Jaji James Odek. upasuaji wabainisha

Mgando wa damu ulisababisha kifo cha Jaji James Odek. upasuaji wabainisha

Kifo cha aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa mjini Kisumu, James Otieno Odek kilitokana na mgando wa damu katika mkuu wake wa kulia. Hayo yamebainishwa na upasuaji uliofanyiwa mwili wa mwendazake leo hii katika Hospitali ya Aga Khan jijini Kisumu na kuongozwa na Mpasuaji Mkuu wa serikali, Johansen Oduor  na kushuhudiwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI vilevile jamaa zake. Imebainika kuwa mgando huo wa damu ulisababisha kuziba kwa msipa mmoja wa kuelekeza damu katika moyo.

Aidha ripoti hiyo imesema kuwa kutokana na kazi ya Jaji huyo ambayo ilimlazimu kukaa chini kwa muda mrefu, huenda ndicho chanzo cha damu kuganda na kusababisha kifo cha ghafla.
 

Odek alipatikana amefariki dunia nyumbani kwake tarehe kumi na sita mwezi huu. Alihudumu katika nafasi ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Huduma za Mahakama, kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa mwaka 2012.

Mwili wa mwendazake unatarajiwa kuzikwa wikendi hii katika Kaunti ya Siaya. Aidha Rais wa Mahakama  ya Rufaa, William Ouko siku ya Alhamisi wiki hii anatarajiwa kutoa mwelekeo wa namna kesi zilizokuwa mbele  ya jaji huyo zitakavyoshughulikiwa. Ikumbukwe Idara ya Mahakama wiki iliyopita ilitangaza kusitishwa kwa shughuli katika mahakama  za rufaa zilizo nje ya Nairobi kufuatia uchache wa majaji kuanzia Janauri kumi na tatu mwaka ujao.