array(0) { } Radio Maisha | DCI yavumbua utapeli mkubwa unaoendeshwa katika Kenya Power

DCI yavumbua utapeli mkubwa unaoendeshwa katika Kenya Power

DCI yavumbua utapeli mkubwa unaoendeshwa katika Kenya Power

Idara ya Upelelezi DCI inatarajiwa kuwasilisha faili kuhusu ripoti ya uchunguzi wa utapeli ambao umekuwa ukiendeshwa katika Kampuni ya Kusambaza Umeme Kenya Power. DCI tayari imekamilisha uchunguzi wake ulioanza mapema mwaka huu na kubaini kwamba waliohusika pakubwa katika ulaghai huo ni wafanyakazi wa ngazi za juu wakishirikiana na wale wa ngazi za chini katika Kenya Power.

Maafisa wakuu akiwamo Kaimu Mkuu wa kitengo cha teknolojia Titus Kitavi, Ambrose Lemanon ambaye ni Kaimu Msimamizi wa Kutengo cha fedha na Benjamin Muoki Mkurugenzi wa Mawasiliano katika kampuni hiyo tayari wamerekodi taarifa.

Aidha uchunguzi katika mifumo ya kulipia ada za huduma za umeme ya Post-Paid na Pre-Paid ulianza mwezi Aprili mwaka huu kufuatilia malalamiko kutoka kwa wateja waliosema kwamba kulikuwapo na kupanda kwa gahrama ya kulipia huduma hiyo, hali ambayo haikuwa kawaida.

Uchunguzi huo umekuwa ukiendeshwa na wataalam wa ukaguzi wa Kenya Power, wataalam wa kukabili ulaghai wa mitanzao  na Kitengo cha Ujasusi katika DCI.

Tayari washukiwa saba ambao ni wafanyakazi wa Kenya Power wa Kitengo cha Teknolojia wameachishwa kazi kwa kuhusika katika utapeli huyo. Kuna jumla ya washukiwa wengine themanini wanaohusishwa, huku wengine kumi wakiomba kuwa mashahidi wa serikali.

Kampuni hiyo iliripoti kupoteza jumla ya shilingi milioni sitini na tano katika mfumo wa kulipia wa Post-Pbaada ya matumizi  huku ikipoteza shilingi milioni thelathini na tano kupitia mfumo wa kulipia wa M-pesa