array(0) { } Radio Maisha | PIGO KWA GORMAHIA, FAIDA YA KWA YANGA
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

PIGO KWA GORMAHIA, FAIDA YA KWA YANGA

PIGO KWA GORMAHIA, FAIDA YA KWA YANGA

Mshambulizi wa Gormahia fc Yikpe Gislein Gnamien huenda akaigura K’ogallo. Taarifa ambazo zinafikia meza ya michezo Redio maisha mapema jumapili ni kwamba raia huyo wa kutoka Ivory Coast ameonekana jijini Daresalaam na wakala wake huku akielekea katika afisi za Yanga fc..

Kwa mujibu wa ukurasa wa Yanga fc ya Tanzania mapema jumapili kwa kupitia mtandao wa facebook ulisema, “Straika wa kutumainiwa wa Gor Mahia raia wa Ivory Coast, Yikpe Gnamien ameshawasili jijini Dar na kupokelewa na Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga SC Thabith Kandorro. Tayari yupo ofisi za GSM, Muda wowote kuanzia sasa atatangazwa kama mchezaji wa Yanga SC!”

Mshambulizi huyo ambaye hajafanya mazoezi na K’ogallo takriban siku nane sasa, mapema siku ya jumatatu alioneshwa kutoridhika na usimamizi wa Gormahia.

“Gor ni timu nzuri, nilikuja hapa na matarajio makubwa lakini kuna uchache wa hela. Japo nafurahia ninapocheza jinsi mashabiki hujitokeza na kuishabikia timu yao, lakini masilahi ya mchezaji lazima yaangaliwe,” alisema Yikpe na idara ya michezo Redio Maisha huku akiongezea kwamba huenda akatafuta ajira kwingine.

Mshambulizi huyo ambaye kwa sasa anachunguzwa kiafya kabla ya kutia saini Yanga fc ametoka nchini Kenya akiwa amefunga ujumla wa mabao mawili katika ligii kuu KPL. Itakuwa pigo kwa Gormahia ambao wana misukosuko ya hela kwa sababu pia mkufunzi Steve Pollack amelalamikia hali mbovu ya kiuchumi na kutishia kuondoka iwapo maswala ya hela hayataangaziwa