array(0) { } Radio Maisha | Francis Kimanzi hana nidhamu, hastahili kuwa Kocha wa Harambee Stars

Francis Kimanzi hana nidhamu, hastahili kuwa Kocha wa Harambee Stars

Francis Kimanzi hana nidhamu, hastahili kuwa Kocha wa Harambee Stars

Katibu mkuu anayeondoka CECAFA , Nicholas Musonye amemkashifu mkufunzi wa timu ya taifa Harambee Stars Francis Kimanzi na kumuita mkosa nidhamu.

Akizungumza na kipindi cha michezo Redio Maisha, Danadana viwanjani siku ya jumamosi mchana, Musonye hakusita kuonesha hisia zake.

“ Mkufunzi wa Harambee Stars ana visababu vingi sana za kutofanya vizuri katika hii michuano. Kwa mfano tulipokuwa Kampala, Uganda alilalamikia hali duni ya viwanja. Kisha baadaye kilicho tukasirisha sana ni kwamba alikuwa anachochea wachezaji kutoheshimu kalenda ya CECAFA. Huyu ni jamaa ambaye hastahili kuiongoza timu ya taifa,” alifoka sana Musonye akiongezea kwamba rais wa shirikisho la kandanda nchini FKF anastahili kumchunguza mkufunzi wake.

Francis Kimanzi alipigwa marufuku ya mechi mbili baada ya mechi ya Harambee Stars dhidi ya Tanzania wakati timu ya taifa ya Kenya iliposhinda mechi hiyo bao moja bila jawabu katika awamu ya makundi.

“Sasa kama wewe ni mtu ambaye una utu, uta jihusishaje na uharibifu wa vyombo katika vyumba vya kubadilikia Kisha baadaye unawachochea wachezaji wako wasicheze mechi ifuatayo Huyo ni mtu ambaye anastahili kuwa kocha wa timu ya taifa kweli” aliuliza Musonye huku akiikemea tabia yake Francis Kimanzi.

Tetesi zasema kwamba Francis Kimanzi aliwafukuza waamuzi wa mechi kutoka katika chumba cha mabadiliko. Kisha baadaye aliwazuia wachezaji wake kwenda kuhekemua kwa muda wa dakika kumi, jambo ambalo lilisababisha mechi hiyo dhidi ya Tanzania kuanza kwa kuchelewa.

Ikumbukwe pia mwaka wa 2011, mwezi Juni tarehe 17 akiwa mkufunzi wa Harambee Stars jijini Lome dhidi ya wenyeji Togo, Kimanzi anasemekana kwamba alimshambulia kwa vita mwamuzi wa mechi hiyo. Jambo hili lilimsababisha yeye kupigwa faini ya shilingi 840,000 na marufuku ya mechi nne wakati huo.

Kwa sasa katibu mkuu wa CECAFA anayeondoka bwana Nicholas Musonye ambaye pia ana malengo ya kusimama kiti cha ugavana katika kaunti ya Kakamega, anamrai rais wa shirikisho la kandanda nchini FKF kumtia adabu kocha mkuu Francis Kimanzi. Kwetu sisi Redio Maisha, twa watakia wote kila la heri katika jitihada zao.