array(0) { } Radio Maisha | Pigo kwa Chelsea, wasiwasi kwa lampard, Nyota akataa kusaini mkataba mpya

Pigo kwa Chelsea, wasiwasi kwa lampard, Nyota akataa kusaini mkataba mpya

Pigo kwa Chelsea, wasiwasi kwa lampard, Nyota akataa kusaini mkataba mpya

Mshambulizi wa Chelsea fc Tammy Abraham amekataa kuzidisha mkataba wake kulingana na ripoti za siku ya alhamisi kutoka Uingereza.

Haya yanajiri baada ya ubora wake wa msimu huu katika ligi kuu Uingereza EPL. Tammy Abraham amefunga mabao 11 katika mechi 16 za Epl msimu huu na mabao mawili katika mechi sita za Klabu Bingwa bara Europa.

Callum Hudson Odoi, Mason Mount, Reuben Loftus Cheek na Billy Gilmour tayari washatia saini katika makubaliano mapya na Chelsea fc.

Odoi kwa sasa ndiye mchezaji ambaye anapokea donge nono kati ya wachezaji hawa waliotokea kutoka akademia. Tetesi Uingereza zasema kwamba Odoi analipwa kwa sasa pauni laki 120 kwa wiki katika makubaliano yake hayo mapya.

Jambo hili linamkosesha usingizi Tammy Abraham ambaye kwa mujibu wa wakala wake anastahili kulipwa zaidi. Abraham  mwenye umri wa miaka 22   ambaye pia ni mshabulizi wa timu ya taifa ya Uingereza, analipwa pauni elfu 50 kwa wiki.