array(0) { } Radio Maisha | KICHAPO CHA MANCITY NICHA AIBU, TUNAHITAJI KOCHA WA KUDUMU

KICHAPO CHA MANCITY NICHA AIBU, TUNAHITAJI KOCHA WA KUDUMU

KICHAPO CHA MANCITY NICHA AIBU, TUNAHITAJI KOCHA WA KUDUMU

Mkufunzi kaimu wa Arsenal fc Freddie Ljungmberg amewahimiza waajiri wake na kuwashinikiza kumtafuta kocha wa kudumu.

Haya yanajiri baada ya Arsenal fc kucharazwa mabao matatu bila kujibu na mabingwa watetezi wa ligii kuu uingereza Manchester City.

“ Si kichapo ambacho waeza jivunia. Si eti kwamba wachezaji wangu hawakutia bidi lakini tukumbuke ya kwamba Man City ni mabingwa watetezi wa EPL. Sisi bado tuko katika harakati za kujitafuta bado. Ni kichapo cha aibu sana. Tunahitaji mkufunzi wa kudumu apewe mkandarasi, hata kama ni mimi au mtu mwingine lakini jambo hili litawatuliza wachezaji kisaikolojia.” Alizungumza Freddie mapema jumatatu, huku akijutia hali ya mibabe hao wa zamani.

Kaimu mkufunzi huyo amelalamika kwa waajiri wake si mara ya kwanza sasa. Baada ya Unay Emery kuondoka, amesalia tu nahodha wa zamani Per Mertesacker ambaye pia ni kocha mkuu wa akademia za Arsenal.

“ Alipo ondoka Emery, aliondoka na jopo kazi lake la ukufunzi. Kwa sasa tuna upungufu wa makocha hapa, ni mimi tu na Mertesacker ambao tuna majukumu ya kuwafunza wachezaji wote wa Arsenal ukiongezea watoto wa akademia. Kamati ya kiufundi ya makocha hapa ina uchache wa makocha. Itabidi wenye klabu hii waajiri mkufunzi haraka iwezekanavyo ambaye pia atakuja na kikosi chake cha ukufunzi,”

Arsenal fc imehusishwa pakubwa sana na aliyekuwa mchezaji wao wa zamani ambaye sasa ni naibu mkufunzi wa Manchester city, mhispania Mikael Arteta. 

Klabu ya Manchester City ambayo inafunzwa na kocha mkuu Josep Guardiola imesema kwamba haitamzuia Arteta iwapo ana nuia kujiunga na Arsenal. Carlo Ancelotti ambaye alifutwa kazi na Napoli sc ya Italia, pia amehusishwa sana na kujiunga na Arsenal fc.