array(0) { } Radio Maisha | FKF WASEME UKWELI, NANI ALIYE PEANA LESENI ZA ‘FIFA CLUB LICENSING’
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

FKF WASEME UKWELI, NANI ALIYE PEANA LESENI ZA ‘FIFA CLUB LICENSING’

FKF WASEME UKWELI, NANI ALIYE PEANA LESENI ZA ‘FIFA CLUB LICENSING’

Kizungumkuti cha leseni za vilabu kwa mujibu wa FIFA katika ligii kuu ya KPL kinazidi kushika moto hasa baada ya utafiti wa idara ya michezo Redio Maisha kubainisha kwamba huenda tukashuhudia vilabu vingine viwili vikishushwa daraja hivi karibuni.

Haya yanajiri baada ya Sony Sugar  maajuzi kushushwa daraja kwa kukosa kuheshimu mechi tatu za kalenda ya KPL. Akizungumza na Redio Maisha mapema Jumanne akiwa afisini mwake jijini Nairobi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Mathare United  Jecktone Obure alionesha masikitiko.

“Tumejaribu kadri ya uwezo wetu lakini bado hali ngumu ya uchumi nchini Kenya inatuburura chini. Hali ya vilabu kama Sony sugar, Chemilil sugar fc, Afc leopards, Gormahia na wengine si yao peke yao. Ni wengi katika ligii kuu nchini wanaumia. Tangu mdhamini mkuu wa KPL ajiondoe, kuna timu yeyote ambaye si ya kampuni inafanya vizuri FKF ambao waliahidi kuisaidia KPL wako wapi Serikali kwa ujumla iko wapi Hawa wachezaji sio wakenya watozwa ushuru hapa nchini” aliuliza Obure kwa majonzi.

Mwaka  2016 baada ya uchaguzi wa FKF, kikosikazi kipya kiki ongozwa na Nick Mwendwa kilichukua hatamu za uongozi FKF. Kabla ya uongozi huo wa viongozi hawa vijana chipukizi ambao wengi walidhania kwamba umejawa na malengo bora, KPL ilidhaminiwa na televisheni ya Supersport na Kampuni ya Mvinyo ya Kenya Breweries. Lakini baada ya muda mfupi tu, kitumbua kikaingia mchanga na sasa kusalia na bora malengo badala ya malengo bora.

“Wazo la FIFA ‘club licensing’ lilikuwa ni wazo bora zaidi maanake hata sisi katika uongozi tulitamani sana KPL iafikie viwango kama vile vya Afrika kusini na mataifa mengine yaliyo stawi. Lakini jiulize ilikuwaje Supersport wakajiondoa

Kenya Breweries wakatoweka Kisha baada ya wao kuondoka FKF nayo ilichukua hatua zipi za kuiokoa KPL isizame ‘Club licensing’ sasa kwanzia hapo imekuwa ni mchezo wa danganya toto maanake wale wote waliotoa stakabadhi za kuonesha kwamba wanastahili kuwa katika ligi, wanaonekana kuwa ni waongo kwa sasa katika wakati huu mgumu. Ni nani huyo ambaye aliyewapatia hivyo vyeti Mbona FKF bado kimya kimya” alimaka sana Obure

Kulingana na Afisa huyo, Shirikisho la Kandanda nchini FKF pamoja na Tume Huru ya Maafisa kutoka Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni FIFA, kwa pamoja walistahili kuhakikisha ya kwamba leseni za vilabu vinahakikisha haki na ukweli ili kuboresha mchezo wa kandanda nchini.

“ Bila ukweli basi tunadanganyana. Hao maafisa wanastahili kuwa wanafanya misako ya dharura kuhakikisha kwamba vilabu vina viwanja, maofisi na miundo misingi mingine ambayo inahitajika. Wengine waliposikia kwamba maafisa hao wanakuja kwa ukaguzi walitafuta maofisi bandia, vilabu vingi nchini havina hata viwanja vya mazoezi. Wachezaji hata wakiumia, hakuna bima.” Alijutia Obure.

FKF maajuzi ikiongozwa na Rais Nick Mwendwa imeonekana kuwa katika hali ya vita na Wizara ya Michezo. Katibu mkuu katika Wizara hiyo Kirimi Kaberia naye alimjibu Mwendwa kwa kutilia shaka jinsi fedha zinavyo tumika katika FKF.

“Kwa mfano timu yangu Mathare United inahitaji milioni 60 kila msimu kuhakikisha mambo yatatuendea uzuri bila mushkil wowote. Lakini ona mdhamini tuliyempata ametupa shilingi milioni 20 peke yake. Kwanzia mwaka jana nimebisha milango na kuandikia makampuni 39 barua za kuomba udhamini bila mafanikio. Kwa nini serikali isi ingilie kati sasa kwa sababu FKF wameonekana kuwa hawana haja na KPL” tandabelua hili liliendelea kuwa kizungumkuti huku Obure akiwaza na kuwazua.

Mchezo wa kandanda nchini Kenya unaonekana kudorora kila uchao. Ligii kuu KPL ambayo ilikuwa na timu 18 kabla ya Sony Sugar kushushwa daraja, ukihesabu kila timu wachezaji takriban 25 ambao wamesajiliwa kucheza ligii hiyo utapata wachezaji 450.

Ukiondoa vilabu ambavyo vinadhaminiwa na makampuni kama vile Tusker FC, Bandari , KCB, Western Stima na wanajeshi Ulinzi stars, utasalia na zaidi ya wachezaji 300 ambao wanaumia kiuchumi.

Ikiwa basi hii ndio ajira, si hawa ni wafanyikazi kama vile wengine wowote pale na wanatozwa ushuru Kwa nini basi kilio chao kimegeuka kuwa machozi ya samaki majini

Rais Uhuru Mwigai Kenyatta ambaye kwa sasa ndiye baba wa taifa, itabidi aangalie nyuma na kuichunguza nyumba yake vizuri. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya vyumba ambavyo vinahitaji ukarabati na kumakinikiwa kimaadili. Mojawapo wa chumba hicho ni idara ya michezo nchini haswa ukizingatia mchezo wa kandanda kwa ujumla. Ni matumaini ya kila mkenya ya kwamba chumba cha mchezo wa kandanda kitashughulikiwa