array(0) { } Radio Maisha | Oguna awashauri wananchi kuhifadhi maji ya mvua
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Oguna awashauri wananchi kuhifadhi maji ya mvua

Oguna awashauri wananchi kuhifadhi maji ya mvua

Serikali imetoa wito kwa wananchi kuhifadhi maji ya mvua inayoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali nchini, ili kukabili kiangazi katika miezi ijayo.

Akitoa wito huo, Msemaji wa Serikali Kanali Mustaafu Cyrus Oguna amesema wananchi wanapaswa kuwa wanapanda miti kwa wingi ili kuzuia na kulinda udongo usisombwe na mafuriko. Aidha, amesisitiza kwamba serikali kwa upande wake inaendelea kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji hayo.

Aidha, Oguna ameeleza kuridhishwa kwake na ushirikiano wa taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wahisani waliojitokeza kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko hususan kwenye maeneo la Pokot Magharibi, mjini Voi na Kaunti ya Isiolo, Wajir na Garissa ambayo yameathirika pakubwa na mvua hiyo.

Wakati uo huo, amerejelea kauli yake ya awali kwamba miili ya watu 7 haijapatikana kufuatia maporomoko ya ardhi kwenye eneo la Pokot Magharibi siku tisa zilizopita.

Kauli yake inajiri wakati watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaitaka serikali hususan kwenye Kaunti za Kaskazini Mashariki kuchimba mabwawa ya kuyahifadhi maji ya mvua kwa siku za usoni.