array(0) { } Radio Maisha | Mvua yatatiza shughuli za uchukuzi Jijini Nairobi

Mvua yatatiza shughuli za uchukuzi Jijini Nairobi

Mvua yatatiza shughuli za uchukuzi Jijini Nairobi

Shughuli za usafiri na biashara zinaendelea kutatizika jijini Nairobi kufuatia mvua kubwa inayonyesha. Mvua hiyo imekuwa ikinyesha mfululizo kuanza Ijumaa wiki iliyopita.

Shughuli za usafiri zimetatizika katika barabara mbalimbali huku msongamano ukishuhudiwa wakati wafanyabiashara wakiendelea kulalamikia kuathiriwa kwa shughuli zao za kila siku.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga, ilisema kuwa mvua kubwa itaendelea hadi kesho Jumatano huku Wakenya wakitakiwa kuwa waangalifu kwani huenda kukatokea mafuriko.

Haya yanajiri, huku zaidi ya familia zaidi ya mia mbili zikiachwa bila makao katika Kaunti ya Taita Taveta kufuatia mafuriko.