array(0) { } Radio Maisha | Kongamano la Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuanza Jumatatu, Mombasa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kongamano la Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuanza Jumatatu, Mombasa

Kongamano la Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuanza Jumatatu, Mombasa

Suala la usambazaji wa vitabu vya kusoma katika Shule mbalimbali za msingi humu nchini inatarajiwa kujadiliwa kwa kina kwenye Kongamano la 15 la kila mwaka la Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi KEPSHA jijini Mombasa litakaloanza rasmi kesho.

Mwenyekiti wa Chama hicho Nicholas Githemia amesema kwamba baadhi ya vitabu ambavyo vimekuwa vikisambazwa si vile ambayo Chama hicho kimependekeza kutumiwa na walimu kuwafunza wanafunzi.

Jingine ni kwamba walimu wamekuwa wakilazimika kuviendea vitabu hivyo katika Ofisi za Idara ya Elimu kwenye Kaunti, badala ya kusambaziwa vitabu hivyo.

Kuhusu utekelezwaji wa Mtaala wa Umilisi CBC, Githemia amesema kwamba Chama hicho kinaunga mkono utekelezwaji wake.

Kulingana naye Mtaala huo anatoa nafasi kwa wanafunzi ambao si werevu kimasomo kufanikisha talanta mbalimbali walizonazo hivyo kuwasaidia kupata fursa ya kujiendeleza kimaisha katika siku zijazo.

Kongamano hilo la siku nne litahudhuriwa na Wakuu 7, 500 na litafanyika katika uwanja wa Chuo cha Kenya School of Revenue Administration kilicho eneo la Customs karibu na Bombolulu.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha anatarajiwa kulifungua rasmi kongamano hilo Jumanne.

Katibu kwenye Wizara hiyo Belio Kipsang’, mwenyekiti wa Tume ya Hudma za Walimu TSC Lydia Nzomo na Mkurugenzi wa Baraza la Mtihani wa Kitaifa KNEC Mercy Karogo ni miongoni mwa watakaolihutubia.

Chama hicho cha Walimu kinawakilisha takriban walimu wakuu 24, 000 wa shule za msingi kote nchini.