array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi amefariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi, Makueni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mwanafunzi amefariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi, Makueni

Mwanafunzi amefariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi, Makueni

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini imezidi kusababisha madhara huku mwanafunzi wa darasa la pili akifariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi katika eneo la Kaiti, Kaunti ya Makueni. 

Inaarifiwa maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambayo imenyesha usiku kuch  na kusababisha nyumba yao kuporomoka.

Aidha nduguye mwanafunzi huyo alinusurika kifo japo amepata majeraha madogo na anaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Kilungu. Kisa hiki kinafikisha watatu watu ambao wamefariki dunia tangu jana kwenye eneo hilo la Kaiti.

Jijini Niarobi Huduma katika kitengo kimoja cha Hospitali ya Binafsi ya Aga Khan zilisitishwa baada ya hospitali hiyo kufurika kufuatia mvua kubwa iliyonyehs jana jioni. Aidha shughuli za uchukuzi zimetatizika mapema leo kwenye baadhi ya barabara jijini kufuatia mvua hiyo.

Kwenye Kaunti ya Taita-Taveta wakazi wa mitaa ya Mwakingali , Sikujua,  Sofia na mitaa mingine hasa Msambweni wanakadiria hasara baada ya nyumba kadhaa , mifugo na magari kusombwa na mafuriko.

Kamanda wa polisi kwenye kaunti hiyo Said Kiprotich amewashauri wakazi kuhamia maeneo  salama ili kuepuka athari za mafuriko.

Kisa kibaya zaidi ni cha Kaunti ya Pokot Magharibi ambapo watu zaidi ya hamsini walifariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi, huku zaidi ya wengine elfu kumi kuachwa bila makao.

Hadi sasa mashirika mbalimbali ya kwa ushirikiano na serikali kuu yanaendelea kutoa misaada kwa waathiriwa wa janga hilo, huku mipango ya kuizika mili arubaini na minane amayo imepatikana kufikia sasa ikitarajiwa kuanza leo hii.

Ikumbukwe Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imeonya kuwa Mvua kubw ainayonyesha sehemu mbalimbali nchini itaendelea kwa siku kadhaa.