array(0) { } Radio Maisha | Polisi wawili wamekamatwa kufuatia jaribio la wizi

Polisi wawili wamekamatwa kufuatia jaribio la wizi

Polisi wawili wamekamatwa kufuatia jaribio la wizi

Maafisa wawili wa polisi waliokamatwa kufuatia jaribio lao la kumwibia dereva wa texi wa Uber kutibuka watafikishwa mahakamani kesho.

Wawili hao Ali Shukri Galgali na Abdikadir Daiwo wote wa cheo cha Kosntable wanaarifiwa walimteka nyara dereva huyo na kumlazimisha kukaa katika kiti cha nyuma cha gari lake kisha kufululiza hadi mtaani Eastleigh badala ya Pangani waliovyokuwa wamesema awali, walipoitisha huduma hiyo.

Kulingana na Idara ya Upelelezi DCI jaribio lao lilitibuka wakati gari hilo lilipoharibika na walipojaribu kutoroka kwa miguu ndipo walipokamatwa.