array(0) { } Radio Maisha | Shida ya Harambee Stars ni mabeki kati, Kimanzi atafute wengine
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Shida ya Harambee Stars ni mabeki kati, Kimanzi atafute wengine

Shida ya Harambee Stars ni mabeki kati, Kimanzi atafute wengine

Mkufunzi wa Posta Rangers Sammy Omollo ‘Pamzo” amemhimiza mkufunzi wa timu ya taifa Harambee stars Francis Kimanzi awatafute mabeki kati wengine.

Akizunguma  mapema jumamosi jijini Nairobi kabla Kimanzi hajataja kikosi ambacho kitawakilisha Kenya katika michuano ya CECAFA, Pamzo alionesha matumaini na kikosi chake Kimanzi japo tashwishwi ipo kidogo tu.

“ Kim amefanya kazi nzuri sana, sote tunamjua na kumtambua. Lakini mie katika ukufunzi wangu na amini kwamba iwapo basi nitapata bao la kwanza kabla ya wewe, basi komboa ufe. Kwa vyovyote vile sitakuruhusu wewe upate bao, inaamisha kwamba lazima ulinzi wetu uwe niwa kupigiwa mfano. Harambee stars kwa sasa imepata alama moja kwa mechi ambazo ingestahili kupata alama tatu, wajua shida iko wapi” aliuliza Pamzo huku akitabasamu.

Harambee Stars ilienda saree ya bao moja kwa moja jijini Alexandria na wenyeji Misri katika michuano ya kufuzu kombe la bara Afrika 2021 Cameroun, siku ya alhamisi tarehe 14 mwezi huu. Siku nne baadaye, Harambee Stars walikuwa nyumbani dhidi ya wageni Togo na kwenda saree nyingine ya bao moja kwa moja.

“Unapo ona matokeo haya haswa dhidi ya Togo nyumbani yanakuashiria nini Afadhali upate bao moja kisha ufunge mlango na upate alama tatu, haswa nyumbani. Shida kubwa ambayo tunayo wakenya ni kwamba mabeki wetu wa kati hawana uwiano. Kuna lugha gongana pale na pia tunakosa kiongozi katika safu yetu ya ulinzi. Tunawo wachezaji wazuri ambao Kimanzi anaweza kuwatumia kwa mfano mchezaji wangu Suleiman Ngotho. Ameonesha ukakamavu wa hali ya juu na uongozi pia, angalia anapokuwa uwanjani. Posta Rangers msimu huu imecheza mechi sita bila kufungwa bao lolote kwa sababu yake,” Alimsifia beki wake Pamzo huku akiongezea kwamba uwiano wa Joash Onyango beki wa Gormahia na Joseph Okumu wa IF Elsfborg si mzuri akisema kwamba ule ni mlango wa nyasi.

Harambee Stars iko katika kundi G huku ikishikilia nafasi ya pili baada ya mechi mbili na alama mbili, sawia na Misri katika nafasi ya tatu lakini kuna tofauti ya wingi wa mabao ndio maana Kenya iko juu. Visiwa vya Komoro wako kidedea baada ya mechi mbili na alama zao nne. Togo wana burura mkia wakiwa na alama moja pekee.

“Kuna wasiwasi mkubwa sana iwapo tutaendelea na mabeki hawa wa kati. Idara zingine ziko sawa, shida ni mabeki kati. Togo ugenini huenda wakatushangaza na mashambulizi makali haswa ukizingatia washambulizi wao warefu warefu. Pia Misri mkondo wa pili ambao tutaucheza Nairobi, itabidi tuwe na mbinu ya kumdhibiti Mo Salah. Kisha wachezaji wa timu ya taifa ya Visiwa vya Komoro nao hawatabiriki haswa washambulizi wao wa pembeni na mmoja wa kati ambaye ana urefu wa twiga. Ili tuwe katika nafasi bora ya kufuzu Afcon 2021 lazima ulinzi wetu uwe bora.” Alimalizia Pamzo huku akiwarai wakenya wote kwa ujumla kujitokeza na kuishabikia timu ya taifa.

Matokeo ya kombe la bara Afrika ambayo yaliandaliwa mwakani kule Misri hayakuwa ya kuridhisha. Lakini wakenya bado wana imani na vijana wa nyumbani katika jitihada za kurejesha hadhi ya mchezo wa kandanda kwa ujumla nchini. Mchango wa wachezaji wa zamani kama vile Pamzo ambaye kwa sasa ni mkufunzi ni wa kupigiwa mfano na unatia moyo sana haswa tunapo angalia kesho.