array(0) { } Radio Maisha | Waamuzi wa KPL wanaumia kimyakimya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Waamuzi wa KPL wanaumia kimyakimya

Waamuzi wa KPL wanaumia kimyakimya

Utafiti wa dawati la michezo Redio Maisha, umebainisha kwamba waamuzi wa ligii kuu nchini Kenya KPL wana  nyanyaswa huku waki endelea kuumia kimya kimya na hakuna wa kusikia kilio chao.

Mapema siku ya alhamisi, utafiti huu ulinifikisha mtaa wa Kaloleni, kaunti ya Nairobi, uwanjani Majimbo.

“ KPL siku hizi imekuwa si nzuri sana kama hapo awali. Nakumbuka chini yake Sam Nyamweya waamuzi walikuwa wanalipwa na FKF. Wakati huu ni vilabu vinavyotulipa sisi. Imekuwa hali ngumu kwa sababu hata ligii yenyewe haina mdhamini, asilimia sabini ama zaidi ya vilabu vyetu pia havina hela. Sasa wewe fikiria sisi waamuzi tuna ishi maisha gani” aliuliza Japheth Juma mwamuzi wa KPL baada ya mazoezi yake ya asubuhi.

Kulingana na mpangilio wa KPL, utaratibu wa malipo ya waamuzi ulipangwa na shirikisho la kandanda FKF. Kwa mujibu wa mpangilio huo, kila timu hupaswa kutoa shilingi elfu 25 ambazo zitatumiwa kama malipo ya waamuzi. Kwa pamoja, ina maanisha kwamba ni shilingi elfu 50 ambazo hugawanywa kati ya waamuzi watano kwa kila mechi.

“ Kila mmoja anapaswa kupata shilingi elfu kumi baada ya mechi. Lakini shida sasa ni kwamba kuna timu kama Sony Sugar ama Chemilil ambazo huja uwanjani kisha baadaye wanasema kwamba hawana hela za waamuzi. Kama ni wewe utafanyaje Mashabiki tayari wanasubiri mchezo. Wasimamizi wa vilabu hivi husema kila wakati watalipa baadaye lakini sasa umeshakuwa mchezo wa paka na panya. Ukihesabu hela ambazo tunadai KPL kwa sababu ya vilabu kama hivi ambavyo havina hela, basi tutakata tamaa na kuwacha kazi hii. Kikubwa ni kwamba tunapenda mchezo wa kandanda na kwa sasa tunajitolea tu.” Aliongezea mwamuzi Amin Agik ambaye pia ana amua ligi ya daraja la pili NSL.

Mara kwa mara baada ya mchezo wa kandanda, mashabiki huondoka uwanjani huku wale ambao hufurahi huendelea kushangilia na wale ambao wanajutia wana endelea na majonzi yao. Lakini ni wachache mno washika dau wa mchezo wa kandanda nchini Kenya ambao huwazia waamuzi. Ikumbukwe ya kwamba pia mambo yakienda ubaya uwanjani, maisha yao huwa hatarini.

“ Kama malipo niya kubahatisha hivi, itakuwa ni bima sasa tuwe nayo Kuna mashabiki kama vile wa Gormahia ama wa Afc leopards ambao huwa wahuni. Iwapo  kwa bahati mbaya utajeruhiwa ukiwa kazini na mashabiki hawa, hali itakuwaje sasa Nani atakaye kulipa ama kugharamia matibabu yako Angalia pia maswala ya ufisadi na upangaji wa mechi kwa mfano, haya mambo yatadhibitiwa vipi na kuna wale ambao wana hela na wale huja tu uwanjani kuheshimu Kalenda ya KPL” Aliuliza Juma huku akisikitikia hali duni ya mchezo wa kandanda kwa ujumla nchini Kenya.

Waamuzi ni muhimu sana katika mchezo wa kandanda maanake wao ndio majaji wa mwisho. Hukumu ya mwisho ni wao. Ili mchezo wa kandanda kwa ujumla uwe na upinzani wa haki nchini, lazima majaji hawa washughulikiwe ipasavyo. Matakwa yao, hali zao, mishahara na mazingira kazini ziwe za kupigiwa mfano. Ni matumaini yetu ya kwamba siku moja haki itatendeka. Kutoka kwetu Redio Maisha twa watakia kila la heri.