×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hakuna upinzani KPL, Gor itabeba taji hili tena

Hakuna upinzani KPL, Gor itabeba taji hili tena

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Harambee Stars Tiellen Oguta ameifutilia mbali kauli ya kwamba ligii kuu nchini Kenya KPL ina upinzani wa kutosha wa kuing’atua Gormahia kutoka kileleni.

Akizungumza mapema jumamosi na idara ya michezo Redio Maisha kabla ya mabingwa hao mara 18 wa KPL kumenyana na mabingwa mara nne Ulinzi Stars, katika uga wa Moi, kaunti ya Kisumu, Tiellen alionesha imani.

“Gormahia ni timu ambaye ina ubabe katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati. Hapo awali Tusker fc, Ulinzi Stars na hata Afc leopards walikuwa na upinzani mzuri sana. Lakini kwa sababu za kisiasa na kutojipanga ipasavyo, K’ogallo wametamalaki. Gor ni timu ambaye ina miundo misingi kabambe ukilinganisha na timu zingine nchini,” alisema beki huyo wa zamani wa Sony Sugar fc, Re-union, Kenya Pipeline fc na Gormahia fc.

Tiellen Oguta aliichezea Gormahia kwanzia msimu wa 1999 hadi 2003. Wakati huo pia, alipata nafasi katika timu ya taifa Harambee Stars, japo ikumbukwe kwamba aliwahi kuichezea Harambee Stars akiwa na umri mdogo wa miaka 16, wakati huo katika kitengo cha vijana wasiozidi umri wa miaka 17.

“ Nilianza mapema sana kucheza mpira, shirikisho la kandanda nchini FKF na wizara ya michezo ilikuwa na mikakati mwafaka ambayo ilitupa nafasi za kunawiri. Kule kwetu visiwa vya mfangano, Kaunti ya Homabay kumetoka wachezaji wazuri sana ambao wameichezea timu ya taifa Hambee Stars na vilabu mashuhuri hapa nchini kama vile Gormahia na Kenya Breweries. Ufanisi wa wakati huo ulitokana na miundo misingi bora kama vile tu Gormahia inayo kwa sasa.” Aliongezea Tiellen.

Gormahia msimu huu wanatarajia kulitetea taji lao la KPL na kutwaa ubingwa wa 19. Timu hiyo imeshindwa mechi moja tu kati ya tisa ambazo tayari imesha cheza huku ikizoa alama 24.

“ Lengo letu niku beba ligi. Ni kweli kwamba mimi mgeni nchini Kenya, lakini nina imani na vijana wangu ambao wamejitolea mhanga kuitetea bendera ya K’ogallo. Shida za kiuchumi zipo kote kote, tusije tukatumia umasikini kama chanzo cha kutofanikiwa maishani. Ulinzi Stars wanafadhiliwa na serikali kwa hivyo ni vijana ambao wako sawa, lakini mshikamano wa vijana wangu nina imani utatusaidia kupata alama tatu,” alisema Steve Pollack, mkufunzi wa Gormahia ambaye pia ameshinda tuzo la mkufunzi bora mwezi wa Oktoba kwa mujibu wa wanahabari wa michezo nchini.

Ulinzi Stars wanashikilia nafasi ya tatu baadaya kucheza mechi 11 wana alama 20. Japo Gormahia wana mechi mbili mkononi ambazo hawakucheza kwa sababu walikuwa wana shiriki michuano ya bara Afrika, pengo la alama nne kati yao na wanajeshi si kubwa.

Kwa vyovyote vile, KDF wanafahamu ya kwamba ili kuwabana Gormahia ambao wako kileleni na Tusker fc ambao wako katika nafasi ya pili na alama 21, mechi ya leo ni lazima washinde. Gormahia nawo wanajua kwamba ili kulitetea taji lao bila mushkil wowote, mechi ya leo wasipotata alama tatu basi kitumbua chao kitakuwa kinaingia mchanga mbele ya mashabiki wao wa nyumbani ‘pacho’.