array(0) { } Radio Maisha | Baadhi ya viongozi wa Bonde la Ufa waunga mkono ripoti ya BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Baadhi ya viongozi wa Bonde la Ufa waunga mkono ripoti ya BBI

Baadhi ya viongozi wa Bonde la Ufa waunga mkono ripoti ya BBI

Na Rosa Agutu,

NAIROBI, KENYA, Baadhi ya viongozi wa eneo la Bonde la Ufa wakiongozwa na Aliyekuwa Gavana wa Bomet, Issac Ruto, Mbunge wa Cherangany Joshua Kutuny na aliyewania ugavana katika Kaunti ya Uasin Gishu, Zedekia Bundotich maarufu Buzeki wamejitokeza kuunga mkondo Ripoti ya Jopokazi la Upatanisho BBI, kwa kauli moja.

Issac Ruto amesema kuwa BBI itasaidia pakubwa katika kiwaunganisha Wakenya na kuepusha ghasia kila baada ya uchaguzi mkuu. Wamesisitiza kuwa uchumi wa taifa hauwezi kuboreshwa kabla ya kwanza kusuluhisha mizozo ya kisiasa inayoligawanya taifa kwa misingi ya kikabila.

Kauli hiyo imetiliwa mkazo na Buzeki ambaye ametoa wito kwa viongozi kutotumia mamlaka yao kuligawanya taifa. Buzeki vilevile ametoa wito kwa vyombo vya habari kuendeleza kazi nzuri ya kupeperusha habari bila kuegemea upande wowote.

Kwa upande wake, Kutuny amewakosoa wanaoipinga ripoti hiyo akisema ni jukumu lao wakiwa viongozi kuhakikisha yatakayojadiliwa yanalenga kuboresha maisha ya Mkenya wa kawaida.

Vilevile Kutuny amesema kuwa baadhi ya viongozi wa Bonde la Ufa wamebuni jopo litakalozuru maeneo ya mashanani na kutangamana na  wananchi kujadili BBI, ambalo litaongozwa na Isaac Ruto.