array(0) { } Radio Maisha | 'Tutasimamia uchaguzi mkuu 2022' asema Chebukati

'Tutasimamia uchaguzi mkuu 2022' asema Chebukati

'Tutasimamia uchaguzi mkuu 2022' asema Chebukati

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Tume ya Uchaguzi, IEBC ndiyo itasimamia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 kwa kuwa haitakuwa imekamilisha muhula wake.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema makamishna waliopo kwa sasa wanapaswa kukamilisha kandarasi yao mwezi Januari mwaka wa 2023 hivyo hakuna atakayewashurutisha kubanduka afisini.

Akilenga pendekezo la Ripoti ya Jopo la Upatanishi, BBI kwamba makamishna wanapaswa kuhudumu kwa muhula mmoja wa miaka mitatu na mwenyekiti kusimamia uchaguzi mmoja, Chebukati amesema mapendekezo hayo yanalenga kuwapotosha Wakenya.

Amesema ripoti hiyo ya BBI haitawaathiri makamishna wa sasa hivyo wataendelea na kandarasi zao kwa mujibu wa sheria.