array(0) { } Radio Maisha | FKF yamruka Philemon Otieno kufuatia jeraha akichezea Harambee Stars
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

FKF yamruka Philemon Otieno kufuatia jeraha akichezea Harambee Stars

FKF yamruka Philemon Otieno kufuatia jeraha akichezea Harambee Stars

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Kenya FKF, ameondoa lawama kwa shirikisho hilo na kusema kwamba si jukumu lao kumtibu beki wa timu ya taifa Harambee stars na Gormahia, Philemon Otieno.

Akizungumza mapema mwezi huu katika kikao cha ujumla na wanahabari, Nick Mwendwa alionekana kughadhabishwa na maswali ambayo yanamhusu Philemon Otieno kutoka kwa meza ya michezo Redio Maisha.

“Kwanza kabisa lazima tuelewane na tuyaweke wazi mambo haya. Philemon Otieno anaonekana kuwa si mtu ambaye si msema kweli. Kile ambacho ninacho kijua ni kwamba hakuumia katika kambi ya Harambee Stars wakati wa michuano ya kombe la bara Afrika kule Misri. Ni jeraha ambalo alikuja nalo kambini. Mkufunzi Sebastian Migne alimjaribu na basi akaridhika nayeye ndio maana akamchagua. Yeye mwenyewe aseme wazi wazi alipata jeraha lake wapi Kama ni katika timu yake Gormahia basi arudi huko atibiwe,” alifoka Mwendwa huku akiongezea kwamba si jukumu la FKF kuwatibu wachezaji ambao wanapata majeraha wakiichezea timu ya taifa.

Kulingana na Philemon Otieno, anakiri ya kwamba alipata jeraha mapema lakini halikuwa la kumkosesha usingizi wakati huo. Jeraha hilo alilipata akiiajibikia timu ya taifa Harambee Stars.

“ Nili umia katika michuano ya kufuzu CHAN kati yetu na Taifa Stars ya Tanzania. Wakati huo sikudhania kwamba ni jambo ambalo lingezua balaa baadaye. Niliendelea na mazoezi huku nikipata matibabu mepesi katika klabu yangu Gormahia. Kitumbua changu kiliingia mchanga baada ya AFCON. Ilinibidi nitafute matibabu zaidi maanake kama ninge endelea hivyo basi ninge lemaa na taaluma yangu ya kucheza mpira inge isha hivyo tu.” Otieno alisema huku akiwashukuru baadhi ya wenzake katika timu ya taifa waliomsaidia kuchangisha takriban shilingi nusu milioni ya Kenya ili kugharamia upasuaji wa goti lake. Wenzake hao ni Michael Olunga, Musa Mohammed, Ayub Timbe, Joash Onyango na Teddy Akumu.

Timu ya taifa Harambee Stars ilikuwa na bajeti ya takriban shilingi milioni 244 ambazo zilitumiwa katika maandalizi ya AFCON kule Misri. Wengi wadadisi wa kandanda nchini na hata serikali kwa kupitia wizara ya michezo imesha anza uchunguzi wa jinsi hela hizo zilivyo tumika na FKF.

“ Hata kule uingereza, nenda kawaulize ama ufanye utafiti wako kuhusu mambo haya. Ushawahi sikia shirikisho la kandanda Uingereza FA limemtibu Marcus Rashford wakati anapo jeruhiwa katika michuano ya kimataifa Kawaida klabu yake Manchester United itamshughulikia au sio Ukiniambia nimtibu Philemo Otieno basi wewe hujui jinsi mchezo wa kandanda husimamiwa. Mchezaji yeyote Yule anapo umia katika timu ya taifa, anapaswa kurejea katika timu yake kutibiwa.” Alimaliza Nick Mwendwa.

Kweli kuna kirindanda katika kandanda nchini Kenya. Si wengi ambao watamwelewa Nick Mwendwa katika hali hii, haswa wakati huu.  Mbona FKF haikutenga hata shilingi milioni tano pekee kati ya milioni 244 ambazo zingetumika kwa minajili za matibabu ama dharura nyingine yeyote ile ya kiafya

Kuna faida gani mchezaji kuhudumia taifa lake kisha limtelekeze wakati wake wa haja Basi inamaanisha kwamba uzalendo kwa ujumla kwa wachezaji kandanda siku hizi umekosa maana Philemon Otieno kwa sasa anaendelea na matibabu yake na ana matumaini ya kurejea tena mazoezini na Gormahia mapema Januari mwaka ujao.