array(0) { } Radio Maisha | Mwanamume auliwa Mombasa kwa kujaribu kumpokonya polisi bunduki

Mwanamume auliwa Mombasa kwa kujaribu kumpokonya polisi bunduki

Mwanamume auliwa Mombasa kwa kujaribu kumpokonya polisi bunduki

Idara ya Usalama kwenye Kaunti ya Mombasa imeanzisha uchunguzi kufuatia kisa ambapo mwanamume mmoja ameuliwa kwa kupigwa risasi eneo la Bondeni na afisa wa polisi baada ya jaribio la kumpokonya bunduki kutibuka.

Abdul Hakim ambaye ni mzee wa Nyumba Kumi eneo hilo amesema kwamba mwanamume huyo ambaye hajatambuliwa alimnyang'anya bunduki afisa huyo na kujaribu kumfyatulia risasi japo jaribio hilo likaambulia patupu. Imeulazimu umma kuingilia kati na kumsadia afisa huyo kupata bunduki yake kabla kumuua mwanamume huyo.

Hawa hapa ni wakazi walioshuhudia kisa hicho ambacho kimetokea karibu na Benki ya Gulf. Mwili wa mwanamume huyo umelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General jijini humo.