array(0) { } Radio Maisha | Watu saba hawajulikani waliko tangu kutokea kwa maporomoko ya ardhi Pokot Magharibi

Watu saba hawajulikani waliko tangu kutokea kwa maporomoko ya ardhi Pokot Magharibi

Watu saba hawajulikani waliko tangu kutokea kwa maporomoko ya ardhi Pokot Magharibi

Mili ya watu saba waliofariki kufuatia mafuriko usiku wa kuamkia Jumamosi wiki iliyopita kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi bado inatafutwa, amesema Msemaji wa Serikali Kanali - Mstaafu Cyrus Oguna.

Akihutubu katika eneo la Kapenguria, Oguna aidha amesema mili arubaini na mitatu imepatikana hadi sasa.

Aidha, Oguna amesema serikali kupitia Mamlaka ya Ujenzi wa Barabara, KEnHA imeweka mikakati mwafaka ili kukarabati barabara zilizokatika kufuatia mafuriko.

Wakati uo huo, Oguna amesema barabara mbadala zimetengenezwa ili kutumika na madereva wa magari madogo madogo huku malori yakilazimika kusubiri kwa muda kiasi.