array(0) { } Radio Maisha | Ole Kina asema ripoti ya BBI haiwakilishi maoni ya wananchi waliyotoa

Ole Kina asema ripoti ya BBI haiwakilishi maoni ya wananchi waliyotoa

Ole Kina asema ripoti ya BBI haiwakilishi maoni ya wananchi waliyotoa

Siku moja tu baada ya ripoti ya Jopo la Upatanishi, BBI kuwekwa wazi, viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa maoni yao kuhusu uzinduzi huyo huku baadhi yao wakitilia shaka ripoti hiyo.

Wa hivi punde kupaza sauti yake amekuwa Seneta wa Narok Ledama ole Kina amesema kwamba alikuwa mmoja wa waliotoa maoni yao kwa jopo hilo na kwamba yaliyonakiliwa ni tofauti na maoni yaliyotolewa na asilimia kubwa ya walioshiriki.

Akihojiwa na Runinga ya KTN , Ledama aidha ametilia shaka kipengee ambacho kunampa mamlaka Rais kumchagua Waziri Mkuu akisema kwamba haina tofauti na sasa kwani katika mapendekezo hayo, Rais angali anamamlaka mengi.

Vilevile, Seneta huyo anahofia kwamba huenda kuna njama fiche ya kumrejesha tena ofisini Rais Uhuru Kenyatta wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwani mapendekezi ya BBI hayakuzungumzia lolote kuhusu hatamu za rais anayehudumu kwasasa.