array(0) { } Radio Maisha | Yaliyomo katika Ripoti ya BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Yaliyomo katika Ripoti ya BBI

Yaliyomo katika Ripoti ya BBI

Hatimaye masuala kadhaa yaliyoibuliwa na Wakenya kuhusu mabadiliko wanayotaka nchini kupitia ripoti ya Jopo la Upatanishi  BBI, yamewekwa wazi huku marekebishi ya katiba yakipendekezwa ili kubuni wadhifa wa Waziri Mkuu, kulipwa kwa Wakenya wanaochangia kuwatambua wahusika wa ufisadi vilevile kubanduliwa kwa Tume ya Uchaguzi, IEBC iliyopo sasa na kubuniwa kwa nyingine kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Mapendekezo hayo yamewekwa wazi kwa umma katika Ukumbi wa Bomas katika halfa iliyohudhuriwa na watu zaidi ya elfu nne wakiwamo viongozi wa matabaka mbalimbali, Rais, naibu wake, magavana, wabunge, maseneta, wageni waalikwa na wananchi.

Mojawapo la masuala makuu ni Rais mwenye mamlaka kuendelea kuchaguliwa na wananchi jinsi ilivyo sasa. Aidha, wadhifa wa Waziri Mkuu utabuniwa ambapo atateuliwa na Rais miongoni mwa wabunge na Rais pia atakuwa na mamlaka ya kumfuta kazi. Atakayekuwa wa pili katika uchaguzi wa Rais atawa Kiongozi wa Upinzani bungeni. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Collins Odote alisoma baadhi ya mapendekezo hayo ya wananchi. 

Kuhusu watakaowafichua watu fisadi, Wakenya elfu 7 waliotoa maoni katika ripoti hiyo wanapendekeza wazawidiwe asilimia 5 ya fedha zilizoibwa, ili kuwachochea wengi kuripoti visa hivyo, jinsi anavyoeleza Profesa Partricia Kameli.

Kuhusu suala la viongozi kukatalia madarakani wanapohusishwa na ufisadi, Wakenya wanapendekeza wanaotajwa wajiuzulu nyadhifa zao ili kupisha uchunguzi vilevile ofisi ya msimamizi wa bajeti kupewa mamlaka makuu ya kuisimamia ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha za umma.

Aidha, imependekezwa kuvunjwa kwa tume ya sasa ya IEBC kabla ya 2022, kuondoa ulazima wa mwenyekiti kuwa mwanasheria na makamishna kuteuliwa na vyama vya kisiasa na wanachama wake wasiwe wa kudumu huku tume hizo zikiwajibishwa mara kwa mara kuhusu utendazi wake.

Kufuatia kukithiri kwa visa vya sumu katika chakula kama mahindi, sukari na kadhalika, imependekezwa kwamba mamlaka maalum ibuniwe ili kuangazia ubora wa chakula nchini.

Masuala mengine ni wafanyakazi wa umma kuzuiwa kufanya kazi na serikali, kushughulikiwa kwa tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana vilevile kaunti kupewa mamlaka ya kuzisimamia bajeti zao ili kuhakikisha utendakazi katika kaunti hauathiriwi na ukosefu wa fedha.

Mwenyekiti wa jopo lililoandaa ripoti hiyo, Yusuf Hajji amesema matarajio ya wananchi ni kwamba mapendekezo yao yatatekelezwa wala hayatasahaulika sawa na ilivyofanyikwa kwa baadhi ya ripoti zilizoandaliwa nchini.

Jopo la BBI lilifanya kazi kwa kipindi cha miezi kumi na mitano huku taasisi mia moja ishirini na tatu zikiwasilisha maoni yao na nyaraka mia saba kumi na tano kukabidhiwa BBI zikiwa na maoni ya watu binafsi. Wakenya sasa wameshauriwa kuisoma ripoti hiyo huku kongamano kubwa la kitaifa likifanyika Januari mwaka ujao kutathmini zaidi mapendekezo hayo.