array(0) { } Radio Maisha | Familia zilizoathiriwa na maporomoko Pokot Magharibi zashauriwa kuhesabu idadi ya jamaa zao
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Familia zilizoathiriwa na maporomoko Pokot Magharibi zashauriwa kuhesabu idadi ya jamaa zao

Familia zilizoathiriwa na maporomoko Pokot Magharibi zashauriwa kuhesabu idadi ya jamaa zao

Wakazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi walioathiriwa pakubwa na mafuriko wameshauriwa kuhesabu idadi ya jamaa zao ili kutoa ripoti kwa serikali iwapo kuna jamaa wao ambao hawajulikani waliko, tangu kutokea kwa maporomoko ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini.  Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Pokot Magharibi, ambaye amesema hatua hiyo itafanikisha harakati za kutoa msaada kwa waathiriwa, vilevile kubaini idadi kamili ya watu ambao hawajulikani waliko.  

Hayo yanajiri huku viongozi mbalimbali wakiwatembelea majeruhi kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kapenguria, ambapo pia wametoa rambirambi zao kwa waliofiwa. Waliofika ni Gavana wa Mandera Ali Roba, Gavana wa Marsabit Ali Mohammed Mohamud wakiongozwa na gavana wa kaunti iliyoathirika Profesa John Lonyangapuo.

Lonyangapuo amesema kuwa wahudumu wa afya wamesafirishwa kwa ndege hadi maeneo ya kaunti hiyo ili kuwasaidia waathiriwa huku wahudumu zaidi wakitarajiwa kutumwa kwenye maeneo hayo. Kwa mujibu wa Lonyangapuo, madaktari wawili walipelekwa hapo jana hadi maeneo ya Muino naTamkal.

Hata hivyo, imekuwa vigumu kuzifikia kambi takribani kumi na tano ambazo zinatumiwa na waathiriwa , baada ya barabara katika maeneo ya Kapenguria na Lodwar kuharibiwa na mvua. Jumla ya watu elfu kumi wameachwa bila makao kufuatia maporomo hayo ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.

Wakati uo huo, wakazi wanaoshi kwenye maeneo ambayo si salama hasa nyanda za chini katika kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet, kwa mara nyingine, wameshauriwa kuhamia sehemu zenye miinuko ili kuepuka athari za mvua kubwa.

Kamishna wa kaunti hiyo, Ahmed Omar amesema kuwa maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo tayari yameonesha dalili za kuporomoka akiwashauri wakazi kuhama mara moja.
 
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wamepuuza agizo hilo wakitaka kufidiwa kabla ya kuondoka. Omar amewashuri wakazi hao kuhama ili kuepusha maafa, akiahidi kuwa watshughulikiwa na serikali.
 
Hata hivyo, Mwakilishi wa Wadi ya Soy Kusini Jona Tanui,  ameitaka serikali kuhakikisha kuwa waathiriwa wa mafuriko wanasaidika.
Tanui amesema mwaka wa 2007,  waathiriwa wa mafuriko katika eneo hilo walihamishwa na kufikia sasa hawajapata fidia au msaada wowote kutoka kwa serikali.