array(0) { } Radio Maisha | Ripoti ya BBI yapendekeza kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu mwenye mamlaka
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ripoti ya BBI yapendekeza kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu mwenye mamlaka

Ripoti ya BBI yapendekeza kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu mwenye mamlaka

Huku ripoti ya Mpango wa Upatanishi ikitarajiwa kuwekwa wazi asubuhi hii, imebainika kwamba baadhi ya mapendekezo makuu yanayobashiriwa kuwa katika ripoti hiyo ni pamoja na kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu Mwenye Mamlaka Makuu na manaibu wake wawili.

Aidha, inatarajiwa kwamba ripoti hiyo itapendekeza baraza la mawaziri ambalo litabuniwa kwa ushirikiano wa Rais na Waziri Mkuu na pendekezo la fedha zaidi kutengezwa Serikali za Kaunti. Hii hapa kauli ya Rais Uhuru Kenyatta.

Ripoti hiyo aidha inatarajiwa kupendekeza kuwapo kwa Rais mwenye mamlaka tendaji, ambaye atateuliwa na wananchi, huku atakayeibuka wa pili baada ya kinyang'anyiro cha urais, akiteuliwa bungeni kuwa Kiongozi wa upinzani na ambaye vilevile, anatarajiwa kubuni baraza shindani la mawaziri litakaloshindana KIAIDIOLOJIA yani SHADOW CABINET na mawaziri walioteuliwa na Rais. Aidha Waziri Mkuu atateuliwa na Wabunge baada ya jina lake kupendekezwa na Rais.

Kuhusu muundo wa serikali, Jopo la BBI limependekeza mfumo wa uongozi kwa kimombo “a home grown and inclusive”. Mfumo huo utajumuisha Rais, Naibu wake, Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri. Aidha, Rais atastahili kupata asilimia 50 au zaidi ya kura zitakazopigwa wakati wa uchaguzi mkuu na au asilimia 25 za kura zote, ambazo zitapigwa kwenye kaunti  takribani 24. Rais vilevile atasalia kuwa kiongozi wa taifa na amiri Jeshi Mkuu.

Naibu wa rais, kulinga na ripoti ya BBI, atasalia kuwa msaidizi wa Rais na mgombea mwenza wakati wa uchaguzi.Kinyume na uvumi ulioenezwa na baadhi ya wanasiasa, ripoti hiyo inaarifiwa kwamba haijapendekeza kuongezwa kwa mawaziri ama kuanzishwa kwa mfumo wa bunge. Wawakilishi wadi watasimamia hazina ya ufadhili wa masomo mashinani  mbali na kufuatilia kwa karibi utendakazi wa magavama.

Viongozi watachguliwa katika serikali za kimaeneo watashili kuwateuliwa wanawake kuwa manaibu hao ikiwa njia moja yawapo ya kufanikisha usawa.