array(0) { } Radio Maisha | Dunia kuadhimisha siku ya uhamasisho dhidi ya dhulma za kijinsia

Dunia kuadhimisha siku ya uhamasisho dhidi ya dhulma za kijinsia

Dunia kuadhimisha siku ya uhamasisho dhidi ya dhulma za kijinsia

Kenya ikijiunga na mataifa mengine kuadhimisha siku 16 za maadhimisho na uhamasisho kuhusu dhulma za kijinsia hadi tarehe 10 Disemba, mikakati inaendelea kuwekwa kuhakikisha haki za kila mmoja zinaheshimiwa.

Kwa mujibu wa data iliyotolewa na kundi la Femicide Awarenes mitandaoni, mwaka huu pekee wanawake themanini na wawili wameuliwa na waume au wapenzi wao.

Hapo jana Viongozi wa Kike nchini kwa ushirikiano na Wizara ya Huduma za Umma, Vijana na Jinsia, walikashifu vikali dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana wakishinikiza hatua za haraka kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Viongozi hao wakiwamo wabunge, maseneta na wawakilishi wadi, walisema kuwa hivi karibuni, mauaji ya kiholela ya watu wa jinsia ya kike yameongezeka, hatua ambayo inatishia usalama wao.